Steven Charles Kanumba ni staa mkubwa Bongo. Jina lake kwa sasa lina hadhi ya kimataifa. Inawezekana akawa ndiye msanii kijana mwenye mvuto kijamii kuliko mwingine yeyote.
Mvuto wake unatambulika ndiyo maana makampuni mengi ya kibiashara na kijamii hupenda kumtumia kama balozi wao. Kanumba ni fahari ya Tanzania, ni kivutio cha vijana wengi wa kizazi kipya.
Lengo la makala haya ni kumshauri Kanumba. Pamoja na sifa nyingi alizonazo kuna makosa machache huwa anayafanya, hivyo anahitaji kupokea ushauri ambao utamsaidia kuepuka visa vya hapa na pale ambavyo humvunjia heshima.
MATATIZO NI NINI?
Hapa kuna baadhi ya matukio ambayo yamewahi kuripotiwa, hivyo kumchafua Kanumba, kwa hiyo anapaswa kujitenga nayo ili heshima yake ibaki kuwa juu.
MOSI: Ugomvi na aliyekuwa mpenzi wake, Wema Sepetu mpaka kufikia hatua ya kupelekana polisi.
TATU: Alizama kwenye dimbwi la mahaba (kama alivyodai mwenyewe) na Miss Ilala 2003, Nargis Mohamed. Walipoachana, alifunguka kuwa mrembo huyo ambaye kwa sasa ni mke wa mtu, alikuwa anamtesa sana.
NNE: Anadaiwa kuwa na uhusiano wa siri na Aunt Ezekiel (ingawa wote wanakanusha), juzikati walitibuana, kisha yeye alimpa mitama mrembo huyo na kusababisha soo hilo litinge polisi.
ISHU IKOJE?
Kwa nini kila siku ugomvi na wanawake? Inakuwaje polisi na yeye kwa makosa ambayo yana alama za kimapenzi?
Daktari aliye pia bingwa wa saikolojia, Godfrey Chale aliiambia Showbiz kuwa tatizo linalomsumbua Kanumba linaitwa Personality Disorder na tiba yake ni ushauri na nasaha.
“Personality Disorder ina matawi mawili, inferior (kujihisi unyonge) na superior (kujiona unahitaji kuogopwa). Vitu hivyo hutengeneza wivu na migogoro mingi (conflicts).
“Mtu kama huyo atakuwa anajiona superior, kwa hiyo hujikuta ana chembechembe za dharau kwa kuamini ni maarufu na ni lazima mpenzi wake amnyenyekee. Ikiwa atakutana na hali tofauti, mfano akigundua mwenzi wake hafuati anavyotaka au anamsaliti, kwa kawaida hujisikia vibaya.
“Ile tabia ya kujiona superior ndiyo humfanya ashindwe kukubali matokeo hasi kutoka kwa mwenzi wake, kwani anaamini yeye ni mtu wa kunyenyekewa. Kutokana na hilo, ndiyo maana hupata kesi za kugombana au kusumbuana na wapenzi wake kwa sababu ya kutokubali matokeo,” alisema Dk. Chale ambaye ana hospitali binafsi, pia hutoa ushauri wa afya kupitia magazeti ya Global Publishers.
Dokta Patrick Mirumbe wa Hospitali ya Capricorn alisema: “Tatizo lake ni wivu. Hiyo naweza kuzungumza kwa kifupi na tiba yake ni ushauri na nasaha. Akipata ushauri wa kutosha anaweza kubadilika na kuwa mtu safi.
KANUMBA ASHIKE NINI?
Mwanasaikolojia ambaye hutoa ushauri wake kwenye magazeti ya Global Publishers, Richard Manyota alisema kuwa jambo ambalo Kanumba anapaswa kushika ili kuepukana na vitu ambavyo vinaweza kushusha heshima yake ni kujitambua.
“Katika makundi ya saikolojia, lipo linaloitwa Legal Psychology. Hili linamtaka mtu atambue mazingira anayoishi na ufahamu wake. Kanumba anatakiwa ajijue yeye ni mtu maarufu na heshima yake ipo juu, kwa hiyo asipojitambua itakuwa tatizo sana.
“Namuomba Kanumba ajijue yeye ni nani, awe mwepesi kuepukana na shari ndogo ndogo ambazo mwisho wake huwa ni mbaya, kama kupelekana polisi. Nadhani akijitambua, akiwa mwepesi kuelewa dalili za ugomvi, ataweza kujirekebisha.
“Anaweza kwenda kwa washauri zaidi lakini hapa mimi nampa kitu muhimu zaidi na akishike. Anaweza kuishi kwa amani maisha yake yote bila migogoro. Akijitambua, hata anapoachana na wapenzi wake, amani itatawala na hakutakuwa na fujo za polisi,” Manyota.
HITIMISHO
Naamini kuwa maneno ya madaktari akiyashika sawasawa pia ushauri wa mwisho wa mwanasaikolojia Manyota, bila shaka atashinda mitihani inayomkabili. Lengo ni kuona heshima yake inazidi kupaa juu na msimamo ni kwamba Kanumba bila polisi inawezekana.
Ninachokiona mimi hapo Kanumba feels SUPERIOR anataka hao wadada washuke chini mara zote wamnyenyekee yeye tuu, anasahau kuwa mwanamke anahitaji kubembelezwa pia, halafu kibaya zaidi anao date nao pia ni ma 'super star' - hakika mafahali wawili hawakai zizi moja.